Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara

Unahitaji msaada wa Maths-Whizz? Umefika mahali sahihi…

Je, ninaweza kutumia Maths- Whizz kwenye iPad au tablet?

Ndio. Kutumia Maths-Whizz kwenye iPad au tableti yako, pakua programu ya elimu inayopatikana bure na ambayo ni salama, Puffin Academy Browser.

Pakua kupitia Apple App Store  

Pakua kupitia Google Play Store

Mara baada ya kupakua, fungua Puffin Academy na bofya Home page kufungua Puffin Academy Portal. Kisha, tafuta 'Maths-Whizz' na bofya kitufe cha 'Install'.

Maths-Whizz sasa imewekwa kwenye iPad au tableti yako. Watoto wako wanaweza kuipata Maths-Whizz muda wowote, mahali popote palipo na huduma ya mtandao, kwa kubonyeza kivinjari cha Puffin Academy.

Kwa matokeo bora zaidi ya kujifunza, tunashauri kwamba watoto watumie Maths-Whizz kwenye kompyuta mpakato au kompyuta ya mezani.

Tunamaanisha kwa tathmini ya kwanza?

Tathmini ya awali kwa ufanisi husoma kwa ufupi uwezo wa sasa wa hisabati wa kila mwanafunzi mada kwa mada. Hii huwasilishwa kwa mtindo wa mtihani na unaweza kugawanywa kwa masomo muingiliano. Tathmini ya awali hutambulisha kiwango cha awali cha ugumu kwa kila mtoto, hivyo ni muhimu kwamba watoto wasisaidiwe wakati wa kufanyiwa tathmini. Tathmini ni lazima ikamilishwe ili kuona ripoti ya mtoto.

Ni kwa jinsi gani amana hupatikana?

Kila somo lina thamani ya amana 15, wakati kila mtihani una thamani ya amana 30. Unaweza kupata amana hadi 10 kwa kuishinda alama yako ya awali na muda wa mfumo Marudio. Amana zinaweza kutumika katika Duka la Whizz.

Umri wa Hisabati ni nini™?

Umri wa Hisabati™ ni istilahi ya kipekee kwa Maths-Whizz ambayo hufasili uwezo wa hisabati, sawa kabisa na ‘Umri wa Kusoma’ unaosaidia kufasili uwezo kusoma. Tunatuma malengo ya mwaka wa kundi ili kukokotoa Umri wa Hisabati™ kuelekea robo ya mwaka ya karibu kabisa (k.m Umri wa Hisabati™ 8.25 = sawa na uwezo wa hisabati wa umri miaka nane na robo).

Ni nini mahitaji ya chini ya mfumo yanayohitajika ili Maths-Whizz kuweza kufanya kazi?

F Explorer 7.05, Kiwango cha 10.3181.22, Firefox 4.0.1
Ikiwa unatumia tarakilishi ya Mac na kuona skrini tupu au umekumbana na tatizo la kuganda, tafadhali tumia Mozilla Firefox badala ya Safari kuipata tovuti yetu.

Mahitaji ya Programu:
Internet Explorer 7 au mpya zaidi au
Mozilla Firefox 4 au mpya zaidi;
Flash Player 10 Plugin au mpya zaidi.

Mahitaji ya chini ya Tarakilishi:
Pentium II 400 MHz au AMD K6-2 au 100% prosesa sawa
Windows 98, 2000, ME au XP
64Mb RAM
16 bit rangi (ingawa 32 bit ndo inapendekezwa)
Kadi ya sauti na vipaza sauti (muhimu kwa Hatua ya 1, sio lazima kwa Hatua ya 2 na kuendelea)
Tunapendekeza ukubwa wa chini wa skrini kuwa 1024 x 768 pixels

Mahitaji ya chini kwa MAC:
G3, G4 Mac 300MHz
Mac OS X toleo la 10.1 na 128Mb RAM au Mac OS 8.6 au 9 na 64Mb RAM
Kivinjari pendekezwa: Mozilla Firefox. Ikiwa unatumia Safari 5, huenda ukapata matatizo kwenye flash Player. Ikitokea hivyo tafadhali tumia Mozilla Firefox au Camino.
Tunapendekeza uwe na mtandao wa broadband ili kutumia Maths-Whizz

Kwa nini siwezi kuingiza majibu? Kwa nini masomo yanaganda?

Tafadhali hakikisha kuwa pop-up blocker imefungwa au haifanyi kazi, kwani itakuwa ikiingilia na utendaji kazi wa programu. Pia angalia kama unatumia toleo jipya la Adobe Flash.

Je Maths-Whizz inafuata mtaala?

Ndio. Maths-Whizz inafuata mtaala wa Kenya. Tafadhali wasiliana nasi kwa maelezo zaidi.

Somo moja linajirudia rudia, ninawezaje kurekebisha hii?

Unahitaji kufuta 'cache' au 'historia' ya kivinjari chako. Wakati mwingine hii hufahamika kama 'faili za muda mfupi' na mara nyingi hupatikana chini ya mapendekezo au orodha ya chaguzi kwenye kivinjari chako.

Ni mara ngapi Maths-Whizz itumike?

Tunapendekeza kwamba wanafunzi wengi watumie Maths-Whizz kwa dakika 45-60 kwa wiki, na wale wanaohitaji msaada zaidi watumie kwa dakika 90 kwa wiki. Tumegundua kuwa vipindi vya dakika 20-30, mara 2-3 kwa wiki, hutoa matokeo bora zaidi.

Jinsi gani naweza kutuma ujumbe kwa darasa langu au mwanafunzi maalum?

Ingia kwenye akaunti yako zindua Ripoti, kisha fungua Ripoti ya Darasa. Kisha, chagua ikoni ya bahasha kwenye kona ya juu ya upande wa kulia wa ukurasa kufuata maelekezo. Tafadhali kumbuka kwamba wanafunzi hawawezi kujibu ujumbe huu.

Jinsi gani naweza kuweka upya nywila au tarehe ya kuzaliwa ya mwanafunzi?

Tafuta darasa ambalo mwanafunzi yupo kwenye ukurasa wa Muhtasari wa Akaunti na kisha chagua penseli na ikoni ya karatasi karibu na jina la mwanafunzi. Ingiza mabadiliko yako kisha bofya 'hifadhi.'

Ni miaka gani kundi Maths-Whizz inashughulikia?

Kwa ujumla Maths-Whizz inashughulikia maudhui kuanzia Msingi hadi mwaka wa 8. Wateja wanapata maudhui yote.

Jinsi gani muda wa matumizi unavyokokotolewa katika Maths-Whizz?

Ni muda tu uliotumiwa katika Mfumo Mkufunzi na Marudio ndio huhesabiwa kama matumizi. Sehemu ya mafunzo ya somo haihesabiwi kama matumizi, muda huanza pale mwanafunzi anapoulizwa swali la kwanza katika kila somo. Wanafunzi lazima wakamilishe somo zima au mtihani ili matumizi yaweze kurekodiwa na kuonyeshwa katika ripoti zao.

Mwanafunzi wangu hajui kusoma bado, je anaweza kutumia Maths-Whizz?

Ndio, masomo yote anayolenga Msingi hadi hadi Mwaka 2 yana sauti hivyo si lazima kujua kusoma.

Jinsi gani Maths-Whizz inabinafsisha maelekezo?

Maths-Whizz inatumia tathmini ya awali na kisha kuendelea kuwafanyia tathmini wanafunzi mara kwa mara kwa kutumia masomo na kwa kutumia vituo maalumu vya ukaguzi ndani ya mtaala. Mfumo wetu endelevu wa tathmini huwezesha Maths-Whizz kubinafsisha maelekezo kwa kila mwanafunzi, ambao huyaelewa masomo yetu na huchochea ukuaji kulingana na kasi pamoja na msaada unaotolewa kwa mahitaji ya kipekee ya kila mwanafunzi. Jinsi wanafunzi wanavyofanya kazi kwenye mtaala, Maths-Whizz hujibu haraka – huku ikifuatilia wanafunzi na hivyo kuweza kuendelea.

Kwa nini masomo ni rahisi sana kwa mwanafunzi wangu?

Sababu kuu ya masomo kuwa rahisi sana ni kwamba mwanafunzi alikosa maswali mengi mno au alikuwa akibofya kitufe cha 'Sijui bado' wakati wa kufanyiwa tathmini ya awali.

Ufumbuzi:

  1. Mfanyie mwanafunizi tathmini tena. Hakikisha mwanafunzi wako anajua kwamba tahtmini anayofanyiwa inatumika kuamua nafasi yake katika Mkufunzi. Mwanafunzi anapopewa changamoto sahihi, kujifunza huwa kunafurahisha zaidi.
  2. Mjulishe mwanafunzi wako kwamba atapokea amana zaidi kwa maswali aliyojibu kwa usahihi wakati tathmini. Mara nyingi hii huwahamasisha kujaribu kwa bidii.

  3. Mwache mwanafunzi wako aendelee kufanya kazi kupitia masomo yaliyotolewa. Ugumu wa somo unaendana na jinsi mwanafunzi anavyofanya. Kama majibu ni sahihi, kiwango cha ugumu huongezeka.
Kwa nini masomo ni magumu sana kwa mwanafunzi wangu?

Kunaweza kuwa na sababu kadhaa ambazo zinazosababisha masomo yanayotolewa kuwa magumu sana kwa mwanafunzi wako.

  1. Mwanafunzi aliepewa msaada, mbali na ule unaotolewa ndani ya Mkufunzi, wakati alipokuwa akifanyiwa tathmini au kwenye masomo. Ni kawaida kutaka kumsaidia mwanafunzi hasa pale tunapodhani anashindwa kujibu maswali. Hata hivyo pamoja na nia njema tuliyonayo, Maths-Whizz inahitaji kujua ni nini mwanafunzi haelewi kama inavyohitaji kujua ni nini mwanafunzi anaelewa - hii ndiyo njia pekee masomo sahihi yanaweza kutolewa.
  2. Mwanafunzi anasumbuliwa na au amechoka.


Ufumbuzi:

  1. Mwambie mwanafunzi akuelezee kile kinachoulizwa kwenye swali. Wakati mwingine kuzungumza na wanafunzi huwasaidia kuelewa kile kinachoulizwa.

  2. Pata mapumziko - wakati mwingine mapumziko mafupi ni suluhisho la kila kitu. Rudi kwenye Maths-Whizz baada ya mapumziko mafupi na au baada ya kupata vitafunwa.

  3. Kama somo ni gumu sana, mwache mwanafunzi ajibu kwa makosa. Mtoe hofu mwanafunzi ili ajue kwamba si vibaya kukosea. Maths-Whizz italandanisha mtaala na sehemu anazohitaji kuboresha ili kusaidia maendeleo ya mwanafunzi wako.

Jinsi gani naweza kuruka somo?

Nenda kwenye Dashibodi, chagua ‘Simamia madarasa', teremka chini ili umpate mwanafunzi na utapata kitufe cha 'Ruka' katika sehemu ya Vitendo. Tafadhali soma ushauri kuhusu wakati wa kuruka zoezi. Ni muhimu wanafunzi waweze kukamilisha masomo yote waliopangiwa katika safari zao za kujifunza.

Angalizo: Huwezi kuruka mtihani.

Ni vipi Vigezo na Masharti yenu?

Kwa shule, tuna mikataba mitatu ambayo tutakuomba kusaini wakati unapojisajili kwa mara ya kwanza na Maths-Whizz. Kwanza ni, Vigezo na Masharti yetu ya kutumia Maths-Whizz Plus kwa Shule na pili ni, Mkataba wetu wa Upatikanaji wa Rasilimali za Walimu wa Maths-Whizz.

Zaidi ya hayo, ujio wa GDPR una maana kwamba wote wawili Whizz Education na shule wamekuwa Wadhibiti wa Data zinazohusiana na taarifa binafsi za walimu na wanafunzi wa Maths-Whizz. Tukizingatia hilo, unapojisajili na Maths-Whizz, shule yako pia italazimika kuingia kwenye Mkataba wa Kushirikiana Data na sisi. Kama wewe ni mteja wetu wa awali utakuwa umeshapata mkataba huu kutoka kwetu, wakati watumiaji wote wapya watahitajika kutia sahihi wakati wanapojisajili kwa mara ya kwanza.

Kutazama mikataba hii, tafadhali tembelea ukurasa wetu wa Mikataba ya Usajili.

Je, unahitaji maelezo zaidi ya haya?

Kama una maoni au maswali zaidi, tafadhali omba taarifa zaidi, piga simu +254 734 774 972.